Yanga inaingia kibaruani katika Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo kukabiliana na Singida United kutoka Singida.
Mechi hiyo Yanga itakuwa inacheza bila ya Kocha wake Mkuu, George Lwandamina ambaye amerejea kwao kimyakimya Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United.
Uongozi wa Zesco jana ulitangaza kumrejesha rasmi Kocha wake Lwandamina ambaye alikuwa akiifundisha Yanga.
Kikosi hicho kitakuwa kinaikabili Singida United ambayo iliwaondosha Yanga kunako Kombe la FA kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Mechi itaanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 Maoni:
Post a Comment