Tanzania imezidi kudidimia chini katika viwango vya soka Duniani ambavyo hutolewa na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Kwa sasa Tanzania ipo nafasi ya 160 Duniani ikiwa imeshuka kwa nafasi 16 baada ya awali kuwa katika nafasi ya 144 kabla ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe uliopigwa Harare Novemba 13 mwaka huu.
Stars ilipoteza kwa magoli 3-0 dhidi ya Zimbabwe mchezo ambao ulikuwa unatambuliwa na kalenda ya FIFA na moja kwa moja hii ndiyo sababu kubwa ya Tanzania kuendelea kudidimia chini kwenye viwango hivyo vya ubora wa soka Duniani.
Barani Afrika, Tanzania inakamata nafasi ya 48 huku Argentina ikiendelea kuongoza viwango hivyo kwa level ya Dunia.
0 Maoni:
Post a Comment