
Michuano ya kombe la mabara
itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili ya kundi A kuchezwa, wenyeji
Urusi watashuka katika dimba la Otkrytiye Mjini Moscow, kucheza na
Ureno .
Na mchezo wa pili wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano hiyo timu ya Cameroon watashuka katika dimba la Fisht Olympic kupepetana na New Zealand , mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia.

Urusi ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama tatu baada ya kupata
ushindi dhidi ya New Zealand, Ureno na Cameroon wao wana alama moja moja
na New Zealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.
0 Maoni:
Post a Comment