Abdul Nondo akiwa Mhakamani
Wakili wa Nondo upande wa kulia mwa Abdul Nondo Chance Mloga
Awali Nondo (katikati) akisubiri kuingia mahakamani
Awali Wakili wa Nondo Chance Mloga akiteta na ABdul Nondo kabla ya shughuli za mahakama kuanza
Na Dajari Mgidange,
Leo tarehe 10 April 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) na
Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo amefika mahakama ya Wilaya ya Iringa kwaajili ya kusikiliza maelezo ya
awali kuhusu kesi inayomkabili.
Akisoma mashtaka Upande wa Jamhuri Wakili wa
Serikali Abel Mwandalamo amesema kuwa Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambalo
la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijiji Dar Es Salaam na
kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi
kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Nondo amekana mashtaka hayo yanayo mkabili mbele ya
hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Iringa Hakimu John Mpitanjia.
Aidha upande wa Jamhuri unakusudia kuleta mashahidi
watano ambao ni Copro Salum, Veronica Fredy(Mpenzi wa Nondo), Alphonce Mwamule,
Copro Abdulkadir na mtu kutoka Mtandao wa Tigo.
Kadhalika, upande wa jamhuri unakusudia kuambatanisha
vielelezo vya ushahidi ambavyo ni Taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano
ya simu, Maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo
cha simu za mkononi.
Upande wa Jamhuri umeomba kuanza usikilizwaji wa shauri
hilo na watakuwa tayari kuleta mashahidi baada ya wiki moja.
Naye Hakimu John Mpita Njia amehairisha kesi hiyo na
kuanza kusikilizwa tena mfululizo tarehe 18 na 19 kutokana na maombi ya upande
wa utetezi wakili Chance Mloga kuiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo kwa
mfululizo.
0 Maoni:
Post a Comment