Mganga
wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa
kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani Shinyanga ameuawa
kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) alikwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio
hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano
asubuhi.
Alisema
Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya
kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la kulia na kupigwa
kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria mkononi.
“Watu
hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo kujaribu kumbaka
mwanamke (jina linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya
ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata
mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda
Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na
uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya
kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na
ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo.
0 Maoni:
Post a Comment