Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10 baada ya kujikokota na kuishinda Manchester City kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 yaliyoleta ushindi wa jumla wa Liverpool 5-1 Man City.
City walianza vizuri wakati walipojaribu kulipa deni la 3-0 walizofungwa katika mechi ya kwanza.
Ilikuwa dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Raheem Sterling alimwanzishia Gabriel Jesus aliyeitumia nafasi hiyo kupachika bao la kuwapa matumaini Man City.
Hata hivyo baada ya tukio la vurugu kabla ya muda wa mapumziko lililoisha kwa Meneja Pep Guardiola kuondoshwa katika eneo la benchi la ufundi, City hawakuweza kuyafikia matamanio yao.
Roma imefanya maajabu baada ya kuwabamiza Barcelona 3-0 na hivyo kutinga nusu fainali za mabingwa Ulaya kwa faida ya goli la ugenini.
Barca walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na kuingia uwanjani wakiwa na akiba ya magoli, ambapo kutokana na mechi ya kwanza waliyoipiga Roma bao 4-1, Roma ilikuwa inalazimika kuifunga Barcelona 3-0.
Goli la Edin Dzeko dakika za awali za mchezo (6'), na Penalty ya Daniele de Rossi katika kipindi cha pili dakika ya 58 yamekamilishwa na Goli la Mlinzi Kostas Manolas alilofunga zikiwa zimesalia dakika nane tu mechi kufikia mwisho zimewafanya Barcelona pamoja nakuwa na Lionell Messi ambaye hakufurukuta, kuondokakichwa chini katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
0 Maoni:
Post a Comment