Mwanafunzi Abdul Nondo ameiandikia barua Mahakama ya Iringa kuomba kubadilishiwa mwendesha mashtaka wa kesi yake Hakimu John Mpitanjia.
Nondo ambaye anashtakiwa kwa makosa mawili ya
kudanganya kutekwa na kutoa maelezo ya uongo kituo cha Polisi Mafinga, amesema
kuwa haridhishwi na mwenendo wa kesi yake na anazo hoja 5 ambazo ameziwasilisha
mahakamani hii leo kuomba kubadilishwa kwa hakimu.
Amesema amekuwa akimuona Hakimu Mpitanjia akiwa na
RCO wa wakiwa ofisini na kupanda gari lake jambo ambalo limepelekea yeye kuhisi
kwenda tofauti na kesi yake Mahakamani hapo.
Sababu nyingine amesema kuwa Hakimu huyo amekuwa
akimuuliza shahidi namba tatu upande wa Jamhuri kuhusu mawasiliano yake na shahidi
huyo hali ambayo anatilia shaka kutotendeka kwa haki katika kesi hiyo.
Upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa
Serikali Abel Mwandalamo ameiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo kutokana
na kukosa ushahidi wa maombi yaliyoelezwa na upande wa utetezi.
Hakimu Mpitanjia amesema kuwa amesikiliza pande
zote mbili na amehairisha kesi hiyo mpaka Tarehe 16 ya mwezi huu ambapo atakuja
na majibu ya kutoendelea kusikiliza kesi hiyo au la.
Naye Mratibu wa haki za Binadamu Nchini Onesmo
Olengurumwa amesema mtuhumiwa Abdul Nondo anayo haki kisheria kuomba
kubadilishiwa mwendesha mashtaka endapo anahisi kutotendeka kwa haki wakati wa
kesi yake.
0 Maoni:
Post a Comment