Tume ya Ulaya imeupiga faini mtandao
wa kijamii Facebook ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni miamoja na
ishirini kwa kutambua kwamba walikuwa wakiwapa maofisa wa umoja wa Ulaya
taarifa potofu wakati walipokuwa wakinunua app ya ujumbe mfupi wa
maneno wa WhatsApp mnamo mwaka 2014.
Tume hiyo imesema kwamba
wakati wa makubaliano hayo tathimini iliyofanywa ilithibitisha kuwa
hakutakuwa na muunganiko baina ya mtandao wa kijamii wa Facebook na
akaunti za WhatsApp , hata hivyo mtandao huo uliendelea kuwapa wateja
uchaguzi wa nini cha kufanya na hivyo kutokuwa na kizuizi.
Kamishna
wa tume hiyo ya Ulaya, Margarethe Vestager, amesema kuwa hatua hiyo
dalili kwamba kampuni zinapaswa kutoa taarifa sahihi.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment