Real Madrid imefanikiwa kufuzu kungia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa mabao 4-3 kwa njia ya Aggregate.
Madrid imekubali kichapo cha mabao 3-1 usiku na kufanya idadi ya mabao kuwa 4-3 hivyo kuipa nafasi ya kusonga mbele mpaka nusu fainali.
Juventus walijipatia mabao kupitia kwa Mandzukic aliyefunga mawili na jingine likifungwa na Matuidi.
Wakati mpira ukiwa umebakiza dakika tatu za nyongeza kumalizika, Real Madrid walipata tuta ambalo lilileta mzozo baina ya refa wa mchezo na kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon.
Mzozo huo ulipelekea Mwamuzi kumpa kadi nyekundu Buffon na kutoka nje kisha ambapo Juventus waliamua kufanya mabadiliko ya kumtoa mchezaji mmoja na kumuingiza kipa Wojciech Szczęsn ambaye alishindwa kucheza penati ya Ronaldo iliyoipeleka Madrid nusu fainali.
Licha ya kulazimishwa sare ya 0-0 leo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Bayern Munich imesonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi Sevilla.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Spain, Bayern iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na leo mechi ya marudiano imemalizika kwa suluhu ya kutofungana.
0 Maoni:
Post a Comment