Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Juma Masenza akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
Afisa habari Mkoa wa Iringa Denis Gondwe(Kulia) pamoja na waandishi wa Habari wa Mkoa huo
Na Dajari Mgidange, Iringa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi Mkoani Iringa kuanzia
kesho tar 29 mwezi huu mpaka tar 4 mwezi wa tano mwaka huu.
Katika taarifa yake na waandishi wa habari na
Mtandao huu dmgidange.blogspot.com Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Juma Masenza
amesema kuwa wanatarajia kumpokea Rais Magufuli jumapili ya tarehe 29 mwezi huu
kuanziaa saa 3 asubuhi katika kijiji cha Ndolela Wilaya ya Iringa ambapo
atasomewa Taarifa ya Mkoa sambamba na kuzindua Barabara ya kutoka Kijiji cha
Migori kwenda Fufu ambayo pia inakatiza mjini Iringa.
“Tarehe 1 mwezi Mei Rais Dr John Pombe
Magufuli atakuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi
ambapo Kitaifa yanafanyika Mkoani hapa na kutakuwepo na viongozi mbalimbali
akiwemo waheshimiwa Spika wa Bunge na Naibu wake, Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Waheshimiwa wabunge na wengine wengi”. Amesema Masenza.
Wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Mei Mosi mkuu huyo wa Mkoa wa Iringa amewaomba wananchi wote kujitokeza kwa
wingi na kuwahi mapema asubuhi kumlaki Rais Magufuli katika uwanja wa samora
mjini Iringa ambapo maadhimisho hayo yatafanyika uwanjani hapo.
Aidha katika Ziara nyingine Tarehe 2 mwezi wa
tano mwaka huu Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali
iliyopo wilayani Kilolo ambapo Pia Masenza amewataka wananchi wa Kilolo
kujitokeza kwa wingi katika uwekaji wa jiwe la msingi katika Hospitali hiyo ya
Wilaya.
Kadhalika tarehe 3 mwezi huu siku inayofuata
Rais Magufuli atazindua kiwanda cha Silverlands ikifuatiwa na uzinduzi wa
barabara ya Iyovi Mafinga katika eneo la Ihemi Wilaya ya Iringa vijijini.
Baada ya Ziara hizo Rais Magufuli anatarajiwa
kuondoka Mkoani Iringa tarehe 4 mwezi wa tano mwaka huu.
Ujio wa Rais Magufuli Mkoani Iringa ni wa
kwanza tangu achaguliwe na wananchi kuwa Rais mwaka 2015.
TAARIFA ZINGINE ZINAZOENDELEA KUSOMWA
0 Maoni:
Post a Comment