Kesi
inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo imehairishwa leo mpaka tar 27 mwezi huu kutokana na upande wa Jamhuri
kuomba muda wa kujibu hoja za upande wa Utetezi.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya upande wa
Jamhuri kuiomba Mahakama kupokea kielelezo cha ushahidi wa nakala ya
mawasiliano yaliyokuwa kwenye simu ya Nondo.
Upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili
Jebrah Kambole ulipinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kutokana na kielelezo hicho kuambatanishwa na
taarifa za kwenye simu pamoja na Laptop huku ilipaswa kuambatanishwa taarifa za
kwenye simu pekee yake.
Sababu nyingine ambayo upande wa Utetezi
imepinga ni kutokana na vielelezo hivyo kutokidhi vigezo vya Kisheria ya
Electronic Transaction act ya 2015 Kifungu kidogo cha 18
Aidha kwa upande wa Jamhuri umeombwa
kuhairishwa kwa shauri hilo ili kuweza kujiridhisha na hoja zilizotolewa na
upande wa utetezi.
Naye mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Hakimu John
Mpitanjia alikubali ombi hilo na
kuhairisha kesi hiyo mpaka tare 27 mwezi huu.
Awali Mahakama ilisikiliza ushahidi kutoka
upande wa Jamhuri Veronica Sylivester Fredy aliyekuwa mpenzi wa Nondo ambaye
alikili kumtambua Nondo kuwahi kuwa Mpenzi wake lakini waliachana mwaka jana
2017.
Shahidi wa pili ni Detective Abdulkarim
ambaye yupo Makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam kitengo cha uchunguzi wa makosa
ya kimtandao ambaye ndiye aliyetoa kielelezo cha nakala ya taarifa zilizokuwemo
kwenye simu ya Nondo.
Itakumbukwa kuwa Nondo anatuhumiwa kwa makosa
mawili Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018
akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Kosa la pili ni
kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha
Mafinga Wilayani Mufindi.
0 Maoni:
Post a Comment