Na Dajari Mgidange,
Kocha
wa timu ya majogoo wa jiji Liverpool amewataka mashabiki wa timu hiyo kutumia
busara kubwa wakati wa mapokezi ya timu wanayokutana nao kwa mara ya kwanza
mchezo wa nusu fainali ya mabingwa barani ulaya Roma.
Hatua
hiyo imekuja mara baada ya michezo iliyopita dhidi ya Manchester City katika
hatua ya Robo fainali walipokutana mahasimu hao wakati wa mapokezi ya timu hiyo
Anfields mashabiki wa Liverpool walirusha chupa za vinywaji na baruti za moshi.
Klopp
amewataka mashabiki kuwaonesha heshima Roma na kuleta vurugu zozote zile hata
kurusha vitu viatavyowavunjia heshima.
“Hatuhitaji
kurusha vitu vyovyote vile hii Club inaonekana ni kutoka anga la maajabu zaidi
tutafanya vizuri ndani ya uwanja na nje ya uwanja tunahitji kuonesha heshima
tunayotakiwa kuonesha”. Amesema Klopp
Katika
tukio lililofanyika tarehe 4 Mwezi huu dhidi ya Manchester City baadhi ya
Polisi pia walijeruhiwa kutokana na vurugu za mashabiki Liverpool lakini bado
tukio hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi.
Liverpool
ni timu pekee ya Uingereza iliyobakia katika michuano mikubwa zaidi Duniani ya
Uefa Champions na watahitaji ushindi leo wakiwa nyumbani Anfield dhidi wa
wageni wao Roma mchezo utakaopigwa majira ya saa 3:45 usiku.
0 Maoni:
Post a Comment