Kikosi cha Simba kimeanza safari asubuhi hii kuelekea mkoani Iringa ambapo kitaweka kambi ya muda ili kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Suhar FC.
Kikosi kitasafiri kuelekea Morogoro siku ya Ijumaa tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Jamhuri.
Simba inaondoka Njombe ikiwa imevuna alama tatu muhimu ambazo zimeifanua iendelee kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 49.
Baada ya mechi na Mtibwa, Simba itakuwa inakibarua kingine dhidi ya Tanzania Prisons FC ya Mbeya.
0 Maoni:
Post a Comment