Wapinzani wa Yanga katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Welayta Dicha FC, wanatarajiwa kuwasili leo nchini.
Kikosi hicho kinatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 6 mchana wa leo kikitokea Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Yanga iliyotoka jana jioni, ilieleza uwasili wa timu hiyo iliyopangwa kukipiga na Wanajangwani hao baada ya droo kuchezeshwa na CAF wiki kadhaa zilizopita, utakuwa mchana wa leo.
Yanga itawakaribisha Welayta Dicha FC Jumamosi ya wiki hii katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Tayari Yanga walishaweka kambi maalum mjini Morogoro kwa ajili ya kufanya maandalizi kuelekea mechi hiyo ya kitaifa.
0 Maoni:
Post a Comment