RONALDO AONESHA UBABE KWA JUVENTUS

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa mechi mbili kuchezwa.

Juventus iliyokuwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani iliambulia kichapo cha mabao 3-o kutoka kwa Real Madrid huku Ronald akiibuka shujaa kwa kupachika mabao mawili.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza unaitengenezea mazingira mazuri Real Madrid kusonga mbele hatua ya nusu fainali endapo italinda matokeo yake katika mzunguko wa pili.

Bao jingine la Real Madrid lilifungwa na Marcelo katika mchezo huo.

Mbali na Madrid, Sevilla waliondoa Manchester United 16 bora jana walichezea kichapo cha mabao 2-1 wakiwa kwao Spain dhidi ya Bayern Munich.

Mabao ya Munich yalifungwa na Jesus Navas pamoja na Thiago Alcantara huku bao pekee la Sevilla likifungwa na Sarabia. 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment