Nondo katikati akiwa na mawakili wake
Na Dajari Mgidange,
Mashahidi wawili kati ya
watano waanza kusikilizwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo huku kesi ikihairishwa kutokana na mvutano wa mawakili.
Kesi hiyo ambayo leo mahakama imeanza
kusikiliza upande wa mashtaka ambao wamewaleta mashahidi watano sambamba na
vielelezo vya ushahidi na upande wa utetezi ulikuwa tayari kusikiliza.
Mashahidi wawili kati ya watano walioletwa na
upande wa mashtaka uliowakilishwa na Wakili wa Serikali Alex Mwita akisaidiwa
na Wakili Pienzia Michombe walipata nafasi ya kuanza kusikilizwa ushahidi wao.
Mashahidi hao wawili waliopata nafasi ya kutoa
ushahidi ni wote kutoka Kituo cha Polisi cha Mafinga Wilayani Mufindi ambao ni
E.2328 Copro Salum ambaye alimpokea Nondo na kuandika maelezo yake na Mwingine
ni E.7651 Copro John ambaye ni Afisa upelelezi wa Kituo hicho.
Shahidi wa kwanza ambaye ni Copro Salum
katika kutoa ushahidi wake amesema kuwa Mnao Tar 7 machi mwaka huu majira ya
saa nane mchana aliingia kazini chumba cha mashtaka na akiwa hapo akiendelea na
kazi ndipo majira ya saa moja usiku alikuja mteja aliyejitambulisha kuwa
anaitwa Abdul Mahmudu Nondo akiwa katika hali ya kawaida akiwa na Begi na mfuko
wa Rambo na kumueleza kuwa alitekwa na watu wasiofahamika.
Aidha baada ya hapo Copro Salum amesema kuwa
alichukua jukumu hilo na kukabidhi kwa afisa upelelezi kituoni hapo Detective
John kwaajili ya kumhoji kwa kina.
Kwa upande wake Shahidi namba mbili Copro
John amesema kuwa Mnamo tar 7 mwezi
Machi majira ya saa Moja jioni alipokea maelezo kutoka kwa copro Salum kuwa
kuna kijana ameleta malalamiko kuwa ametekwa ndipo alipochukua jukumu la
kumhoji kwa undani zaidi.
Amesema baada ya kuona swala hilo ni gumu
alichukua jukumu la kumpeleka ofisi ya mkuu wa Upelelezi ambako aliamriwa
kupekua mabegi ya Nondo na kukuta kompyuta ndogo ya Laptop aina ya Dell, Simu
aina ya Itel, Kadi ya Benk na Kitambulisho cha Chuo.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Jumatatu ya
Tarehe 23 Mwezi huu kutokana na Upande wa Utetezi chini ya Wakili Jebra Kambole
na Wakili wa Serikali Alex Mwita kuwa na mvutano juu ya utofauti wa majina yaliyoandikishwa
na Copro John na Copro Salum kuambatanishwa kama vielelezo vya ushahidi
mahakamani.
Itakumbukwa
kuwa Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa
za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao
wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa
mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
0 Maoni:
Post a Comment