Wenger: Meneja kutoka England atashinda EPL

Arsenal Arsene Wenger
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema hivi akribuni meneja mzaliwa wa England atashinda Ligi ya England.
Ni miaka 25 tangu mzaliwa wa England Howard Wilkinson alipoongoza Leeds kushinda taji la ligi mwaka 1992, mwaka mmoja kabla ya Ligi ya Premia kuanzishwa.
"Sidhani kama tutakaa miaka mingine 25," alisema Wenger na kuongeza kwamba kuna mameneja wengi sana wa England ambao wameonesha matumaini.
Wenger, ambaye ameshinda taji la ligi mara mbili akiwa na Arsenal tangu achukue usukani kutoka kwa Bruce Rioch mwaka 1996, alisema: "Sidhani hili ni tatizo la England, linatokana na hali kwamba Ligi ya Premia ina ushindani mkubwa sana kimataifa na leo klabu zote kubwa zina mameneja kutoka nje.
"Awali, mameneja wengi kutoka Scotland walishinda mataji England. Tuna mameneja wengi sana wa England ambao wameonesha amtumaini.
"Shriikisho la soka la England limefanya kazi nzuri katika kutoa mafunzo kwa wakufunzi na karibuni tutashuhudia mabadiliko.
"Nilipowasili, nakumbuka kulikuwa na makala nyingi watu wakisema mameneja wa kutoka nje hawangewahi kushinda ubingwa wa lihi.
"mambo yatabadilika tena, nina uhakika, tumefikia wakati wa mabadiliko historia ya soka England na mameneja wa England watashinda Ligi ya Premia."
Wenger pia alitetea wachezaji wake ambao wamekosolewa kwa kuonyesha urafiki kupita kiasi na wachezaji wa Manchester United kabla ya mechi ya Jumapili.
Na pia, ametoa pole zake kwa mshambuliaji Lucas Perez ambaye amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza msimu huu.
Gunners watakutana na Southampton mechi ya Ligi ya Premia uwanjani St Mary's Jumatano, akifahamu kwamba iwapo watashinda basi watapanda juu ya Manchester United hadi nafasi ya tano, alama tatu nyuma ya Manchester City walio nafasi ya nne.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment