Abdul Nondo akiwa Mahakamani leo April 18
Mawakili wa Nondo Jebra Kambole Kulia na Chance Mloga katikati
Kesi
inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi
Tanzania (TSNP) na Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo ambayo ilipaswa kusikilizwa mfululuizo leo April 18, 2018 na April 19 imehairishwa mpaka
kesho kutokana na Hakimu wa kesi hiyo kuwa na kesi nyingi.
Mmoja wa mawakili wa Nondo wakili
Chance Mloga amesema kuwa Hakimu John Mpitanjia aliomba kupumzika kutokana na
uwingi wa kesi alizozisikiliza siku ya leo.
Amesema wamekubaliana Kesi hiyo kusikilizwa tena kesho April 19,
2018 mapema asubuhi huku upande wa Jamhuri tayari ukiwa umeleta mashahidi wanne
wa kesi hiyo.
Nondo
anatuhumiwa kwa makosa mawili Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo
mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa
WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa
mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
0 Maoni:
Post a Comment