Rais wa zamani wa Zimbabwe amesema kuwa hakufikiria kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa angemgeuka na kusimama dhidi yake na amelaani hatua ya Mnangagwa ya kumuondoa madarakani kwa njia ya mapinduzi.
Robert
Mugabe mwenye umri wa miaka 94 aliiongoza Zimbabwe tangu ilipopata
uhuru mwaka 1980 hadi alipolazimika kuondoka madarakani Novemba mwaka
jana.
Amesema:
"Sikuwahi kufikiria hata siku moja kwamba Emmerson Mnangagwa niliyemlea
na kumleta serikalini na ambaye niliokoa maisha yake akiwa gerezani
alikotishiwa kunyongwa, kwamba siku moja angenigeuka."
Mugabe
amesema aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi na kwamba
Emmerson Mnangagwa ametwaa madaraka kwa njia isiyo halali.
Emmerson
Mnangagwa, aliyekuwa makamu wa Rais wa Zimbabwe alifutwa kazi na Robert
Mugabe na kwenda uhamishoni Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini na
kuchaguliwa na Bunge kuwa rais wa nchi hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment