Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji
Manara amesema kuwa hivi sasa Simba na mashabiki wake hawawezi kuwa
wazalendo kwa Yanga bali uzalendo pekee watakuwa nao kwenye timu ya
taifa tu.
Ameyasema hayo mara baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho huku Yanga nayo ikiwa imeondolewa katika michuano ya
Klabu Bingwa Barani Afrika. baada ya timu hizo kuondolewa kwenye
michuano hiyo zote zikiwa ugenini na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Aidha, kutokana na suluhu hiyo, mashabiki wengi walianza kutoa lawama
kuwa timu hizo kwa kuwa zilishindwa kujipanga vyema na kutumia vizuri
uwanja wa nyumbani.
“Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo
ya timu za bongo kutofanya vizuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo
kwa vilabu vyetu, wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na
nikabezwa na viongozi wao, leo ndio mwaujua uzalendo? Nawaambia kwa sasa
tutafanya zaidi yenu, uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa
tu,”amesema Manara
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment