UONGOZI
wa Lipuli FC, umeweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Lipuli
wameweka mikakati ya kushinda michezo miwili ya Mbao na Mwadui iliyopo mbele
yao watakaocheza ugenini.
Mwenyekiti
wa timu hiyo, Ramadhani Mahano amesema wanatambua nafasi waliyopo wasipokuwa
makini kushinda mechi zilizosalia huenda wakawa na wakati mgumu.
Amesema
wametoa mapumziko ya siku chache kwa wachezaji wao, ila wameenda wakiwa na
mikakati ya kupata ushindi katika michezo iliyopo mbele yao.
Mahano
amesema wasipokuwa makini katika michezo hiyo watakuwa katika wakati mgumu.
Kwa
sasa Lipuli inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania
Bara ikiwa na pointi 27 za mechi 22, ikizidiwa pointi 19 na vinara, Simba na
Yanga wenye pointi 46 kila mmoja.
0 Maoni:
Post a Comment