Menaja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema angependa sana Arsenal wasipangwe kukutana na Atletico Madrid ya
Uhispania katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Hii ni baada ya Gunners kulaza AC Milan ya Italia 3-1 (Jumla 5-1) katika hatua ya 16 bora.
Atletico
Madrid wamekuwa wakicheza vizuri na walifika robofainali Europa League
baada ya kuwalaza Lokomotiv Moscow 5-1 mechi ya marudiano.
Nyota
wa zamani wa Liverpool na Chelsea Fernando Torres alifunga mabao mawili
nao Angel Correa, Saul Niguez na Antoine Griezmann wakafunga moja kila
mmoja Alhamisi na kuwawezesha Atletico kupata ushindi wa jumla wa 8-1
Atletico wameshinda Europa League mara mbili na walifika fainali
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili 2014 na 2016 - walishindwa mara
zote mbili.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck (mawili)
na Granit Xhaka naye Hakan Calhanoglu akawafungia Milan bao la kufutia
machozi Alhamisi.
"Bila shaka tungependa kuwakwepa Atletico Madrid," alisema Wenger.
Hata hivyo, alisema hana usemi wowote na wakikabidhiwa klabu hiyo hawatakuwa na budi ila kukutana nao.
Droo ya robofainali - ambapo kuna klabu nane kutoka mataifa manane - itafanyika leo Ijumaa saa 12:00 GMT.
Huu
ulikuwa ushindi wa tatu wa Arsenal katika kipindi cha wiki moja baada
ya kuwalaza Milan 2-0 mechi ya kwanza mjini Milan na pia wakalza Watford
3-0 Ligi ya Premia Jumapili.
Lakini kabla ya ushindi huo San
Siro, walikuwa wameshindwa mechi nne mtawalia mashindano yote - mara
mbili ikiwa mikononi mwa Manchester City.
"Mambo ni mazuri sana leo. Tulihitaji kujikwamua kutoka kwa matokeo yetu," Wenger alisema.
"Inaonesha
jinsi timu ilivyochukua hatua. Tulikuwa na mechi ngumu lakini mwishowe
tulishinda. Tukiwa na matokeo mazuri na jinsi tunavyocheza soka,
mashabiki watatuunga mkono."
0 Maoni:
Post a Comment