DR. MWAKYEMBE SASA KULA SAHANI MOJA NA DIAMOND PLATNUMZ

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha Naibu wake, Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.
Katika maelezo yake Mwakyembe amesema kuwa inawezekana kwasasa Diamond ameanza kulewa sifa na umaarufu alionao mwanamuziki huyo.
Amesema kuwa serikali imekaa vikao vingi na wasanii lakini Diamond hahudhurii kwa hiyo si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe kutokana na umaarufu wake.
“Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake,” amesema Dkt. Mwakyembe.
Hata hivyo, Dkt. Mwakuembe amemshauri mwanamuziki huyo asishindane na Serikali kama ana ushauri basi autoe kistaarabu ambao utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya, kitu ambacho amesema hajafurahishwa hata kidogo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment