CONTE: BARCELONA HAWAJATUTENDEA HAKI KIPIGO CHA 3-0

Antonio Conte and Lionel Messi

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake imepoteza katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".

Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi kuu Uingereza.

Conte alikiri kwamba Messi - aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge - ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili.

Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha mabao100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment