Msanii
Chid Benz na wenzake watano wamewekwa chini ya uangalizi maalum wa
mahakama na jeshi la polisi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Chid
na wenzake jana walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada
ya upande wa Jamhuri kuiomba mahakama kuwaweka chini ya usimamizi maalum
kwa kipindi cha miaka mitatu.
Polisi
wa kituo cha Msimbazi waliwasilisha kiapo na kuiomba mahakama kuamuru
wawekwe chini ya uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na kusaini bondi na
kuwa na wadhamini, ili kuhakikisha hawajihusishi tena na matumizi ya
dawa za kulevya.
Chid
na wenzake hawakuwa na pingamizi lolote kuhusu maombi hayo ya upande wa
Jamhuri. Mahakama iliridhia maombi hayo na kuamuru msanii huyo na
wenzake kuhakikisha wanaripoti katika kituo cha polisi cha Msimbazi mara
moja kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili.
Aidha, kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja.
Chid
Benzi aliwahi kupandishwa kizimbani baada ya kukamatwa Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) miaka miwili mitatu iliyopita
akiwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati.
Msanii
huyo alikiri kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na amewahi
kuhudhuria matibabu katika jumba maalum Bagamoyo (rehab). Hivi sasa
amesema ameachana na matumizi ya dawa hizo zilizomuathiri kwa kiasi
kikubwa
0 Maoni:
Post a Comment