Wabunge
wanane waliofukuzwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,
anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Prof Ibrahim
Lipumba, jana waliondoka vichwa chini baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es salaam kutupilia mbali ombi lao la zuio la kupinga kuapishwa kwa
wabunge wapya.
Uamuzi
huo umetolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Lugano Mwandambo baada ya
kusikiliza hoja zote za pande mbili, ambapo amesema kuwa mahakama
imetupilia mbali hoja za walalamikaji za kuweka pingamizi kutaka wabunge
wapya wasiapishwe mpaka kesi ya msingi isikilizwe.
Aidha,
Mwandambo amesema kuwa mahakama itasikiliza pingamizi la walalamikaji
walilofungua kupinga kufukuzwa uanachama wa chama cha wananchi CUF na
mwenykiti wao Prof. Ibrahim Lipumba.
Katika
maombi yao walalamikaji wanaomba kutoapishwa kwa wabunge wanane
walioteuliwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba
nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao kwa mujibu wa katiba.
0 Maoni:
Post a Comment