Majanga! Lile sakata la tuhuma za kujihusisha na biashara na matumizi ya
 madawa ya kulevya ‘unga’ lililowagusa watu wa kada mbalimbali, wakiwemo
 baadhi ya mastaa wa Bongo kwa majina yao kutajwa kwenye orodha ya mkuu 
wa mkoa, miezi kadhaa iliyopita, limemkumba rafiki wa aliyekuwa mume wa 
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, marehemu Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ 
ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Patrick Christopher ‘PCK’ (29).
BREAKING NEWS
‘Breaking news’ zilizolifikia Habari zote Jumamosi zilieleza kuwa, kufuatia 
tuhuma hizo, mali za msanii huyo ambazo ni nyingi kiasi cha kushangaza 
kutokana na umri wake mdogo, zinadaiwa kukamatwa jijini Dar. Chanzo 
makini kilicho karibu na msanii huyo kilidai kuwa, katika orodha ya mkuu
 wa mkoa wa Dar, jina lake liliingizwa kwenye listi ya kwanza 
iliyotolewa na mkuu huyo, lakini hakuwepo nchini hivyo aliporejea ndipo 
akajaa kwenye mikono ya polisi na sasa kesi yake hiyo, tayari ipo 
mahakamani
“Mali za PCK zinashikiliwa yakiwemo magari matatu, Toyota Prado 
(shilingi milioni 60), Nissan Murano (shilingi milioni 45) na Toyota 
V-Mark (shilingi milioni 32) na nyumba ya ghorofa ya kifahari iliyopo 
maeneo ya Kigamboni (Dar) jirani kabisa na Ufukwe wa Bahari ya Hindi 
huku akaunti zake zote za benki zikifungwa kutokana na kuwa kiasi 
kikubwa cha fedha hadi kesi yake itakapomalizika kwa sababu inasemekana 
mali hizo siyo za halali.
“Unaambiwa sasa hivi jamaa ana hali ngumu mno maana kesi iko Mahakama ya
 Hakimu Mkazi Kisutu (Dar) huku hati ya kusafiria na vitambulisho vyake 
vyote vikiwa vimeshikiliwa na haruhusiwi kutoka nje ya Jiji la Dar.
“Kiukweli jamaa anatia huruma maana unajua mtu ukishazoea maisha ya 
kitajiri na uhuru ni vigumu sana kuwa sawa pale unapokosa hivyo vitu. 
“Mali zake zimekamatwa kwa kuwa inasemekana siyo za halali kwani 
haijulikani anafanya biashara gani ambazo zinaweza kumwingizia kipato 
kikubwa kiasi hicho hivyo anachunguzwa ndiyo maana zinashikiliwa,” 
kilisema chanzo hicho.
 HABARI ZOTE JUMAMOSI LAMSAKA
Baada ya kunyaka ishu hiyo, Habari zote Jumamosi lilimsaka PCK kwa siku tatu 
hadi alipopatikana ambapo alibanwa hadi akakubali kufunguka. Msanii huyo
 anayetamba na Nyimbo za Nitazame Usoni na Sweet Baby aliyomshikisha 
Mwanamuziki Barnaba Elias alikiri mali zake kushikiliwa na akaunti zake 
kufungwa huku akieleza kuwa, hawezi kuzungumza zaidi kwani atakuwa 
anaingilia uhuru wa mahakama.
“Ni kweli mali zangu zimeshikiliwa yakiwemo magari na nyumba iliyopo 
Kigamboni. Pia vitambulisho na hati za kusafiria zimeshiliwa. Siwezi 
kusema ni shilingi ngapi zilizopo benki wala siwezi kuzungumzia sana 
ishu hii maana tayari iko mahakamani Kisutu,” alisema PCK.
NI RAFIKI WA IVAN
Risasi Jumamosi lilimweleza kuwa, lilitonywa kwamba ni rafiki wa 
marehemu Ivan hivyo kumtaka kufafanua juu ya hilo ambapo alifunguka: “Ni
 kweli Ivan alikuwa ni rafiki yangu sana. Ndiye aliyenitoa kwenye maisha
 ya ziro mpaka hivi nilivyo sasa na ukaribu wetu ulikuwa mkubwa sana. 
“Niliishi naye jijini Kampala Mtaa wa Munyonyo (Uganda) kati ya mwaka 
2000 na 2001.
“Mwaka 2002, Ivan alihamia Afrika Kusini, nikabaki Kampala, ilipofika 
mwaka 2004, aliniita huko (Afrika Kusini) nikawa nimehamia. Mwaka 2007 
niliamua kurudi Bongo kwa sababu ndiyo nyumbani na kuanza kujitegemea 
mwenyewe, lakini bado urafiki na biashara zetu ziliendelea na muda 
mwingi tulikuwa wote Afrika Kusini kwenye biashara zetu wiki kadhaa 
zilizopita kabla ya kuumwa na kufariki dunia.
“Nimeanza kuhaso na maisha haya muda mrefu sana. Huwa sichagui kazi ya 
kufanya hivyo nafanya biashara mbalimbali kwa kusafiri nje ya nchi kama 
Uingereza, China, Afrika Kusini na kwingineko. Pia nafanya Muziki wa 
Bongo Fleva.”
MSIKIE MWANASHERIA WAKE
Habari zote Jumamosi lilizungumza na mwanasheria wake anayesimamia kesi hiyo 
ambaye alijitambulisha kwa jina la Musa Ngonyani ambaye alisema mteja 
wake huyo anashitakiwa kwa kumiliki mali haramu. “Kesi inaendelea 
Mahakama ya Kisutu na namba yake ni CC 247/2017 na inaendeshwa na Hakimu
 Kihawa na itatajwa tena Juni 13, mwaka huu.”
MAMLAKA YA MADAWA YA KULEVYA
Akizungumzia kinachoendelea juu ya vita dhidi ya madawa ya kulevya, 
Afisa Habari wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya 
(DCEA), Florence Bahati Khambi alisema kuwa, vita hiyo inaendelea na 
hakuna ambaye atabaki salama, awe muuzaji, mtumiaji au yeyote yul
0 Maoni:
Post a Comment