Makampuni ya Japan yanafahamika kwa kuwa na muda mrefu zaidi wa kazi
pamoja na misongo ya mawazo inayowakabili wafanyakazi wake, na sasa
baadhi yamedai kuwa waajiriwa wapya ambao ni wanyama ‘paka’ na ‘mbwa’
wanaweza kuwa dawa ya matatizo hayo.
Kampuni ya Workaholic inayotajwa kwa kuwa na muda mrefu zaidi wa kazi,
imedai kuwa tangu iwaajiri wanyama hao ufanisi wa kazi umeongezeka.
Wanyama hao huongeza furaha na ‘kampani’ kwa wafanyakazi.
Hidenobu Fukuda, kiongozi mkuu wa kampuni hiyo amesema kuwa amekuwa
akiwalipa mishahara paka na mbwa hao wanaoingia ofisini, na kwamba
anaridhishwa na kazi wanayoifanaya kwani hata baadhi ya wafanyakazi
wamekiri kupunguza msongo wa mawazo.
“Mbali na mishahara, pia huwa ninalipa ¥5,000 ($45) kila mwezi kwa wote wanaoangalia usalama wa paka hao,” alisema Fukuda.
Alisema kuwa watumishi hao wapya ambao kazi yao kubwa ni kuwafariji na
kuwapa kampani wafanyakazi ofisini, wamefunguliwa akaunti kwenye
mitandao ya kijamii
0 Maoni:
Post a Comment