Uamuzi mpya wa Hans Poppe SIMBA


MUDA mfupi baada ya taarifa kutoka ndani ya Simba kuwa Zacharia Hans Poppe amejiondoa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, sasa kuna mabadiliko na habari ni kuwa amerejea klabuni hapo akitaka nafasi yake.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa baadhi ya viongozi ‘wazito’ wa Simba walikutana na Hans Poppe, jana usiku na kuzungumza naye hadi usiku wa manane kabla ya kumfanya abadilia uamuzi wake wa kujiuzulu.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao kilichodumu muda kwa mrefu kwa kuwa kuondoka kwa Hans Poppe katika nafasi yake ni jambo kubwa na ambalo lingekuwa pigo kwa klabu ya Simba kutokana na mchango wake klabuni hapo.
Hans Poppe amekuwa akisaidia Simba katika masuala kadhaa hasa ya usajili ambapo imefahamia amekuwa akifikia hatu ya kutoa fedha zake za mfukoni kwa kuikopesha klabu kama ambavyo wadau wengine kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kifedha wamekuwa wakifanya.
Inaelezwa kuwa Hans Poppe alifikia uamuzi wa kujiuzulu kutokana na kuona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa, huku suala la mkataba wa Simba na kampuni ya Sportpesa ukitajwa kuhusika.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment