Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema mapambano yanaendelea katika michezo yote ijayo ya ligi kwa kuwa lengo lao kubwa ni kupata ubingwa.
Mchezaji huyo ambaye jana alifunga bao la kwanza wakati Simba ikikipiga na Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa, amesema mechi na Lipuli si ya kubeza.
Bocco ameeleza kuwa wanaijua Lipuli vizuri na watahitaji kupambana ili kupata matokeo waweze kutenegeza mazingira mazuri ya kubeba taji.
Wekundu hao wa Msimbazi walifanikiwa kuitandika Prisons mabao 2-0 jana na kufikisha alama 58 kileleni.
Simba itashuka Uwanja wa Samora Aprili 21 Jumamosi ya wiki ikiwa mgeni wa Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
0 Maoni:
Post a Comment