Msimamo wa VPL baada ya ushindi wa Yanga vs Kagera Sugar


Ushindi wa magoli 2-1 walioupata Yanga dhidi ya Kagera Sugar unawafanya wafikishe pointi 62 sawa na Simba lakini Yanga wanarejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kutokana na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Yanga wamecheza mechi yao ya 27 mechi moja nyuma ya Simba ambayo tayari imeshacheza mechi 28 hadi sasa na kubakiwa na mechi mbili kabla ya ligi kumalizika.
Yanga walifunga goli la kwanza kupitia kwa Simon Msuva aliyeunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Geoffrey Mwashiuya dakika ya 38 kipindi cha kwanza. Mbara Yusuph akaisawazishia Kagera Sugar dakika ya 45+5 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.
Obrey Chilwa akaifungia Yanga goli la ushindi dakika ya 58 kwa kuunganisha krosi ya Haruna Niyonzima na kuihakikishia Yanga ushindi pamoja na pointi tatu muhimu.
Kagera Sugar imefungwa na Yanga mechi zote (mbili) za msimu huu na kuichangia Yanga pointi sita, mechi ya mzunguko wa kwanza Kagera Sugar ilikubali kichapo cha magoli 6-2 kwenye uwanja wa Kaitaba kabla ya leo kufungwa 2-1 kwenye uwanja wa taifa.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment