Mwenyekiti kata ya Kitwiru B akiongea na wananchi
Wananchi kata ya kitwiru iliyopo manispaa ya Iringa wameomba uongoza wa kata hiyo kuweza kutokomeza mbwa wanaozurula mitaani maarufu kwa jina la mbwa koko ambao siku za hivi karibuni wamekua tishio kwa maisha ya watoto wao.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ambao uliitishwa kwaajili ya maendeleo ya Kata hiyo na kujadili maendeleo ya kata yao wananchi hao wameuomba uongozi kuleta kikosi kazi ambacho kitaweza kutokomeza mbwa hao.
Peter Sigunga ni Afisa mifugo katika kata hiyo ambaye amekiri kuwepo kwa mbwa hao ambao ni tishio kwa wananchi kwani baadhi yao hawajapitiwa chanjo ya kuzuia kichaa cha mbwa amesema ataleta kikosi kazi hicho kutokomeza mbwa hao.
Aidha Sigunga amesema kwa sasa wana risasi zaidi ya 300 ambazo ni chahce kwaajili ya kutokomeza mbwa hao na tayri wameshaomba kibari kwaaji ya kutokomeza mbwa hao
Amesema wakati wa zoezi hilo hua wanantoa taarifa ya tahadhari kwa wananchi kua wenye hiyo mifugo waweze kuifungia ndani na baadaye wanafika kwa kushtukiza na kuanza kutokomeza hao mbwa
Afisa mtendaji kata wa Kitwiru Simba Nyunza akitoa ufafanuzi kwa wananchi
Agenda mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo ambapo wananchi kuhusu agenda ya barabara walifikia mufaka kwa makubaliano ya kuchanga kiasi cha fedha cha sh. 3000 Ya kukodi buldoza kwaajili ya kufungua barabara za mitaa zitakazopita kwenye mitaa yao.
0 Maoni:
Post a Comment