Baada ya taarifa kuhusu mgawanyo wa fedha za mkataba wa Pogba kwenda United kuvuja kumeibuka jambo jipya, FIFA wameshtushwa na mgawanyo wa fedha za Pogba na wanataka kuana uchunguzi.
FIFA wanaona kuna figisu zinaweza zilifanyika kati ya wakala wa Paul Pogba na Manchester United katika usajili huo, hii imekuja baada ya kugundulika Raiola alipata kiasi cha £41 katika usajili huo.
Kiasi hicho cha fedha ambacho Raiola amekula kinonekana kuwa kikubwa sana na hii kuamua kuwafanya FIFA kutaka kuanza kufanya upelelezi jinsi Pogba alivyokwenda United kwani huenda kuna kanuni zilikiukwa na ndio maana Raiola akala pesa kubwa.
Taarifa zinasema Mino Raiola tayari alishakula £23m baada ya Pogba kutua Manchester United huku taarifa zikidai kwamba kwa muda wa miaka mitano ijayo itabidi Raiola apewe pesa zingine kiasi cha £19m kutoka United.
Taarifa pia zimevuja kuhusu mshahara wa kiungo huyo aliyevunja rekodi ya usajili ya dunia kwamba analipwa £165,588 kwa wiki lakini pia anaweza kuvuna £255 kwa wiki kama United wakibeba Europa.
0 Maoni:
Post a Comment