Juventus watangulia Cardiff, sasa wanaisubiri Atletico ama Real Madrid.

Monaco wamekuwa timu ya 3 katika ligi 5 maarufu barani Ulaya kufikisha mabao 150 msimu huu zingine zikiwa ni Real Madrid na Barcelona hiyo ni kutokana na bao la kufutia machozi la Kylian Mbape dhidi ya Juventus, lakini hiyo haikutosha kwa wao kutoondolewa katika michuano ya Champions League msimu huu.
Monaco safari yao katika mashindano hayo imekwisha usiku wa jana baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Juventus, ikumbukwe kipigo hicho kinakuja baada ya kile cha nyumbani wiki iliyopita walipofungwa bao 2 kwa 0, na sasa wametolewa kwa jumla ya mabao 4 kwa 1.
Alianza Mario Mandzukic kucheka na nyavu za Monaco dakika ya 33, bao hilo la Mandzukic ni bao lake la kwanza katika michuano ya Champions League katika mechi 14 zilizopita katika hatua ya mtoano, mara ya mwisho kufunga katika hatua ya mtoano ilikuwa mwaka 2014 kipindi hicho akiichezea Bayern Munich.
Dani Alves ambaye anaonekana anazidi kuwa bora kadri siku zinavyokwenda alifunga bao la pili dakika ya 45, bao hili linamfanya Alves kuwa mchezaji wa Juventus anayeongoza katika mchango wa mabao katika michuano hiyo, hadi sasa amefunga mabao 3 na kuassist 4 na hii inamfanya kuchangia mabao 7 hadi sasa.
Kwa matokeo hayo sasa Juventus inaingia fainali kwa mara ya 9 katika mashindano ya Champions League na Europa Cup kwa ujumla, lakini wakiwa na kumbukumbu mbaya ambapo mara yao ya mwisho kuingia fainali ya michuano hiyo msimu wa mwaka 2014/2015 walipoteza dhidi ya Barcelona, sasa Juventus wanasubiria mshindi wa mechi ya leo kati ya Atletico Madrid watakaoikaribisha Real Madrid, fainali ya michuano hii itapigwa mjini Cardiff nchini Wales mwezi ujao.

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment