Uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United uliovunja rekodi ya dunia sasa unachunguzwa na shirikisho la soka duniani Fifa.
Fifa imeandika barua kwa klabu hiyo ya ligi ya Uingereza ikitaka maelezo zaidi.
Shirikisho hilo linataka kujua ni nani alyeshirikishwa katika uhamisho huo wa kitita cha pauni milioni 89.3 na ni fedha ngapi zilizolipwa.
Msemaji wa klabu ya Manchester United :Hatuzungumzii kuhusu kandarasi za watu binafsi.Fifa imekuwa na nakala hizo tangu uhamisho huo ufanyike mwezi Agosti.
Pogba anahudumia msimu wake wa pili katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kuondoka katika klaabu hiyo na kuelekea Juventus kwa kitita cha pauni milioni 1.5 mwaka 2012.
Raia huyo wa Ufaransa mara ya kwanza alijiunga na United kutoka klabu ya Ufaransa ya Le Havre 2009 kwa hali ya utata.
Alirudi katika klabu hiyo msimu uliopita kwa kitita kilichovunja rekodi cha Yuro milioni 105.
United pia ilikubali kuilipa Juventus Yuro milioni 5 kwa malipo ya ziada pamoja na gharama nyengine iwapo Pogba atatia saini kandarasi mpya.
Wakati walipothibitisha uhamisho huo, Juventus ilisema kuwa uhamisho huo umeimarisha uchumi wa klabu hiyo na kufikia Yuro milioni 72.6
0 Maoni:
Post a Comment