Machi 8 ya kila Mwaka siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa
ikiwa ni Muitikio wa Azimio la Umoja wa Mataifa huku Tanzania ikiwa ni miongoni
mwa nchi za Umoja wa Mataifa inaungana na Nchi nyingine Kuadhimisha siku hiyo
huku kauli mbiu ikisema Tanzania ya viwanda
wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Bi Wamoja Ayubu ambaye ni
Katibu Tawala wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewaomba wanawake walio
katika Utumishi wa Umma kutumia fursa mbalimbali zilizopo kujiendeleza kielimu.
“Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilikua na
mpango wa kutoa ufadhili wa masomo wa Shahada ya Uzamili kwa watumishi wa Umma
wanawake ambao ulitekelezwa kwa takribani Miaka 8 kuanzia 2008 hadi 2012, kwa
kipindi hicho wanawake 251 walifanikiwa kupata Shahada ya Uzamili katika Vyuo
mbalimbali Nchini Mwetu na wanawake hao wote waliweza kupandishwa vyeo baada ya
kumaliza masomo yao na mimi ni mmoja wapo kati ya hao wanawake”. Alisema Wamoja
Ayubu.
Bi Wamoja alipata ufadhili na kusoma Shahada ya Uzamili
katika Fani ya Usimamizi wa Biashara ambapo alijiunga na Chuo kikuu cha Dar Es
Salaam mwaka 2006 na kuhitimu mwaka 2008 Huku Kabla ya Kupata Shahada ya
Uzamili alikua Afisa Utawala Mkoa wa Pwani na baada ya kuhitimu alinufaika na
Elimu hiyo kwani Aliongeza Ufanisi Kazini na aliweza kupandishwa cheo mpaka
kufikia Katibu Tawala wa Mkoa.
Aidha Bi Wamoja amewaomba watu wote waungane kwa pamoja
kuongeza Jitihada katika kupigania haki za wanawake kwani bado wanakabiliwa na
Changamoto nyingi ikiwemo uelewa mdogo wa masuala mbalimbali hali inayowafanya
kutojiamini.
Wamoja amesema kutokana na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda
wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi, Wanawake wamekua na mchango
mkubwa katika Ujenzi wa Tanzania ya Viwanda hivyo kuna haja ya kuwapa nafasi ya
kutosha na kuendeleza viwanda.
Katika Hatua nyingine Wamoja amewaomba watu wote kusimamia
haki za wanawake hususani Wanaume kwa kuhakikisha wanapata Elimu na wanapopata
nafasi za uzamili waweze kuwasapoti ili kuongeza uelewa na ufanisi wa kazi
katika Utumishi wa Umma.
0 Maoni:
Post a Comment