NA BARAKA LUSAJO
MVUA
zinazo endelea kunyesha
Mkoani Rukwa zimeendelea kuleta
madhara makubwa kwa
wananchi , ambapo mkazi mmoja
wa kijiji cha Tatanda
kata ya Sopa
wilaya ya kalambo
mkoani Rukwa Winifrida Silukala miaka
54 kufariki dunia
baada kusombwa na maji
ya mvua wakati
akitokea shambani kuelekea
nyumbani kwake.
Tukio
hilo la kushangaza
limetokea katika kijiji
cha Tatanda kata ya Sopa
wilaya ya Kalambo mkoani hapa,ambapo mkazi mmoja wa
kijiji hicho winifrida
silukaga miaka 54
kufariki dunia wakati akivuka
kwenye maji yaliokuwa
yamejikusanya na mavua kubwa
inayo endelea kunyesha mkoani
hapa.
Kufuatia hali
hiyo imefanya ofisi
ya mkuu wa
wilaya hiyo kufika
eneo la tukio sambamba
na kuongea na
wananchi juu ya
kuchukua tahadhari kabla
ya tukio kutokea.
Akiongea na
wananchi wa kijiji
hicho mara baada
ya tukio kutokea
katibu tawala wa
wilaya hiyo Frenk
Schalwe, amesema marehemu alipatwa
na kadhia hiyo
wakati akiwa ametokea shambani kwake
ambapo baada ya
kufika katikati maji yalimzidi
nguvu na hatimaye
kusombwa na maji
hayo .
0 Maoni:
Post a Comment