RC Masenza akizungumza na Waandishi wa Habari
Afisa habari Mkoa wa Iringa Denis Gondwe akichukua maelezo
Baadhi ya waandishi wakichukua habari
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza amesema kumekua na matatizo mengi yakiwa yamesababishwa na vinywaji aina ya Viroba, moja ya matatizo hayo ni ajari za bodaboda lakini nguvu kazi ya Taifa huku uhalifu kama ubakaji pamoja na ukatili wa kijinsia.
Masenza amewataka wanaouza Bar, Glocery pamoja na store mbalimbali za vinywaji kuachana na uuzwaji wa viroba kwani kufanya hivyo ni kinyume na maagizo ya serikali kwani tayari limeshapigwa marufuku.
Aidha Masenza amewaomba wafanya biashara hao kutokomeza vinywaji ambavyo tayari wako navyo katika store zao au maeneo yao ya biashara bila ya kuangalia hasara watakazo pata kwani walipewa muda wakuweza kuzuia kuingiza vinywaji hivyo na hakuna muda wakuongeza tena kwa wafanya biashara hao.
Sanjari na hilo Mkuu huyo amesema hakutakua na msamaha kwa ambaye atakutwa akiuza viroba au kutumia vinywaji hivyo kwani sheria itachukua mkondo wake kwa kukamatwa na kushitakiwa sehemu husika.
"Madereva bodaboda na wengine wamekua wakiendesha vyombo vyao huku wakiweka viroba midomni na kuvifyonza barabarani hali kadhalika kwa wanafunzi ambao wamekua wakiingia darasani wakiwa wamekunywa viroba na kupoteza umakini wa usikivu darasani". Alisema Mh Amina Masenza.
Masenza amesema kama Mkoa wamejipanga vizuri kukabiliana na matumizi hayo ya viroba kwa kufanya Operation mbalimbali katika maeneo mbalimbali hadi vijijini kwa kutumia askari kwa kukusanya vinywaji hivyo pamoja na wauzaji wa vinywaji hivyo.
Aidha Masenza amewaomba wanairinga kushirikiana kutoa taarifa kwa yeyote yule ambaye watamuona akiuza au kusambaza viroba katika maeneo yao kwani anajua kua vinywaji hivyo vitaendelea kuuzwa kwa usiri mkubwa.
0 Maoni:
Post a Comment