ZAIDI YA HEKITA 250 ZA FYEKWA NA MALI ASILI



Na, BARAKA LUSAJO 

WANANCHI   wa  kijiji  cha  Ilimba  kata  ya  Mkoe   wilaya  ya  Kalambo  mkoani Rukwa  wamelalamikia   kitendo  cha  kuendelea  kufyekwa mazao yao  na   wakala  wa  huduma  za mistu  Tanzania  {TFS}   na  huku  zaidi  ya  hekta  250  zikifyekwa kwa  madai  ya  kuendesha  shughuri za  kilimo   ndani  ya   hifadhi  ya misitu  bila  kibari.

Hatua hiyo  inakuja  baada ya  wakala  wa  huduma  za  mistu  Tanzania   {TFS}   mwaka  2013  kuwagiza  wananchi  wa kijiji   cha ilimba  kuacha  kufanya  shughuri  za  kilimo  ndani  ya  hifadhi  inayo  zunguka  kijiji  hicho  na  kuendelea  na  shughuri  hizo  kwa  madai  kuwa   sio   eneo  la  hifadhi na  kupelekea    mamlaka  hiyo   kuchukua  hatua  ya  kufyeka  mazao  yote   ya  wananchi.
Hali  hiyo   imefanya  wananchi  wa  kijiji  hicho  kuitisha   mkutano  wa   hadhara  ili kujua  hatima  ya  mazao  yao,.Ambapo  wamesema  eneo  hilo  wamekuwa  wakilitumia    tangia  miaka   mingi  katika  shughuri  za  kilimo  na  kushangaa   mamlaka  hiyo   kufyeka  zaidi  ya  hekta  250  za mahindi  hali  ambayo  imewapa  hofu na mashaka  kutokana  na  eneo  hilo  kulitegemea  kiuchumi.

Mwenyekiti  wa  kijiji  hicho  Chales  stephano , ambae  licha  ya  kukili   kuwepo  adha  hiyo amesema  zaidi  ya  hekta  250  za mahindi  zimefyekwa  na wakala  wa   huduma  za misitu  Tanzania   {TFS}.

Mtendaji  wa  kijiji  hicho Filibet Fwamba, mbae  licha  ya  kukili  kuwepo adha  hiyo ,emesema  wanawasiwasi   wananchi  wa  kijiji  hicho  kukosa   chakula   katika  msimu  ujao kutokana na mazao  yote  kufyekwa.

 Meneja   wa  huduma  za  misitu  Tanzania {TFS}  Samweli   matula  wilaya  ya  kalambo mkoani   hapa  ,ambae  licha   ya  kukili  kuwepo adha  hiyo  amesema   wananchi   hao  walingia    hifadhi  na kufanya   shughuri  za kilimo bila    kibari   na  kupelekea   mamlaka  kuwafukuza  na  kufyeka  mazao yao na  zoezi   bado  lina endelea.

Hifadhi   hiyo  ilianzishwa  mwaka   1957  kwa  lengo   la  kuhifadhi  vyanzo  vya  maji ,  ambapo  mwaka  2013  wananchi  wote   kwenye  maeneo  hayo waliamuliwa   kuacha  kufanya   shughuri  za  kilimo  na   mwaka  2017    huduma  ya  misitu   Tanzania iliweka  bikoni  kuzunguka  maeneo  hayo ili  wananchi  kutambua   mipaka  ya  hifadhi  hiyo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment