MWAKA MMOJA JERA KWA WIZI WA KUKU

 

MAHAKAMA ya mwanzo mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi Mkoani Songwe,imamuhukumu kifongo cha mwaka mmoja Braun Cheyo (18) mkazi wakijiji cha Ihanda wilayani humo kwa kosa la wizi wa kuku wawili majike mali ya Jackob Menad.

Akisoma shitaka hilo namba 54 ya mwaka 2017 mbela ya hakimu wa mahakama hiyo,mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi,Nurdin Manga ni kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe1/2/2017 majira ya saa 1 jionikatika kijiji cha Ihanda,huku akijua kufanya hivya ni kosa kisheria.

Amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 265 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ambapo alivunja kanuni hiyo kwa kuiba kuku mbili wenye thamani ya 20,000.

Manga amemuomba hakimu wa mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo ambao wanapenda kujipatia mali kwa njia ya wizi badala ya kufanya kazi.

Hakimu wa mahakama hiyo,Edgar Mwaiswaga,ameridhika na ombi la mwendesha mashitaka kabla ya kutoa hukumu alimtaka mtuhumiwa huyo kujitetea au kutoa ombi lolote,ambapo mshitakiwa hakuwa na ombi lolote huku akisubiri maamuzi ya mahakama.

Baada ya mtuhumiwa kukosa neno lolote la utetezi kusema,ndipo hakimu wa mahakama hiyo,alipotoa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela na kumtaka atakapo maliza kifungo hicho atalazimika kuli 20,000,thamani ya kuku hao wawili aliowaiba.

Nje ya mahakama,wananchi waliokuwepo mahakamani hapo,walimpongeza hakimu huyo kwa kutoa adhabu hiyo,wakisema itakuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na kusema kuwa vijana wengi hasa kipindi hiki cha mvua wamekuwa wakivizia majumbani mwa watu na kuiba kuku.

Mwisho.

JELA MWAKA MMOJA KWA WIZI WA PIKIPIKI.

Na Ibrahim Yassin, Mbozi

MAHAKAMA ya mwanzo mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoa Songwe,imempandisha  kizimbani  na kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela Alex Stebu (21) mkazi wa kijiji cha Itaka kata ya Ipunga wilayani humo kwa kosa la wizi wa pikipiki mali ya Elia Mkodya mkazi wa kijiji na kata ya Igamba.

Akisoma kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2017 mbela ya hakimu wa mahakama hiyo,mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi,Nurdin Manga ni kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 265 kanuni ya adhabu sura ya 16.

Amesema mshitakiwa huyo,aliiba pikipiki aina ya T,beter  yenye namba za usajili T 254 CMS yenya thamani ya 1,460,000/ mnamo tarehe 3/2/2017 majira ya saa 11 jioni mali ya Mkodya katika kijiji cha Itaka huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Manga alimuomba hakimu huyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa pikipiki vinavyofanywa na vikundi mbalimbali vya vijana waliojiingiza katika wizi.

Hakimu wa mahakama hiyo,Masia Sang”oro alilidhika na ombi la mwendesha mashitaka na kumtaka mshitakiwa kujitetea au kutoa neno lolote kabla ya kutoa hukumu ambapo mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye ni yatima ametengwa na ndugu na ni mgonjwa .

Kufuatia utetezi huo,hakimu wa mahakama hiyo,alimuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kama fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kupenda kujipatia mali kwa njia za wizi.

Hakimu Gang”olo,alitoa adhabu hiyo ya kumtia hatiani kwa fungu la 37 (i) ya sheria ya mahakimu ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.        
                                                                                                                                                                           
Nje ya mahakama,wananchi waliohudhuria mahakamani hapo waliipongeza mahakama hiyo kwa kutoa adhabu hiyo na kusema itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo na kusema kumekuwa na vitendo vya uporaji wa pikipiki katika wilaya hiyo ambapo watu wengi wameuawa na wengine kujeruhiwa.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment