Kocha
Ronald Koeman wa Everton amesema baada ya kipigo cha mabao 3-0 wakiwa
nyumbani dhidi ya Tottenham katika Ligi Kuu England, sasa wanastahili
ushindi dhidi ya Atalanta.
Everton
itakuwa ugenini kuibaa Atalanta ya Italia katika mechi ya Europa League
kwenye Uwanja wa Mapei na Koeman amesema ni nafasi nzuri kwao
kurekebisha makosa.
Kikosi cha Everton kinadhaminiwa na SportPesa na kilifanya ziara nchini wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUWA
Atalanta (3-4-3): Berisha; Toloi, Palomino, Masiello; Hateboer, Freuler, Cristante, Castagne; Kurtic, Petagna, Gomez
Everton (4-2-3-1): Pickford; Holgate, Keane, Williams, Baines; Schneiderlin, Gueye; Klaassen, Rooney, Sigurdsson; Calvert-Lewin
0 Maoni:
Post a Comment