MWANAFUNZI WA MIAKA 15 ABAKWA.

 

NA BARAKA  LUSAJO

MWANAFUNZI   wa  kidato  cha    kwanza    katika  shule   ya   sekondari  zengwa  kata  ya   legeza  mwendo   wilaya   ya   Kalambo  mkoani  Rukwa   mwenye umri   wa  miaka  15  amejikuta  kwenye  wakati  mgumu  baada  ya  kuvamiwa    wakati  akifua nguo  za  shule  kisha  kubakwa na  Nelsoni  gelvas  miaka  25 mkazi  wa kijiji  cha  mombo.

Tukio  hilo  la  kushangaza  limetokea    katika  kijiji  cha  mombo  kata   ya  legeza  mwendo   wilayani  hapa, ambapo   kufumba  na  kumbua    binti   huyo akiwa  anafua  nguo   za  shule nyumbani  kwao alijukuta  akivamiwa  na  kijana    aliye fahamika  kwa  jina   la  Nelson  gelvas  mwenye umri  wa  miaka  25  kisha  kumbaka.

Mtendaji  wa   kijiji   hicho  Bahati  hapas , amekimbia  kituo  hiki  kuwa    baada  ya  kujitokeza  kwa   kelele  za    kuomba  msaada  kutoka  kwa  binti  huyo,  walimua  kufika  eneo  la  tukio  na kumkuta  binti  huyo akiwa  amebakwa  na  kusema  tukio  lilitokea  wakati  akifungua  nguo za shule.

Mtendaji  wa   kata   hiyo   Laiko  msigwa ambae  licha  ya  kukili  kutokea   tukio  hilo  amesema   baada  ya  tukio  walitoa  taarifa  polisi   ambao walifika  na  juhudi  za  kumsaka  mtuhumiwa   bado  zinaendelea.

Diwani  wa  kata  hiyo  mwakyusa  lameki  Sinjera  , ambe  licha  ya  kukili  kutojea  tukio  hilo amesema   mtuhumiwa  amekatwa    na mpaka  sasa  wanasubiri  kufikishwa  mahakamani.

 Mkuu  wa  wilaya  hiyo   Julith  binyura  amekili  kutokea   tukio  hilo, na  kusema  tayari  mtuhumiwa   amekamatwa  na atafunguliwa   kesi  mahakamani  na  kuwataka  wazazi  kujitokeza  kutoa   ushahidi  bila   kupindisha  ili  kutokomeza   vitendo  hivyo.

 

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment