Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi
juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa
za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa
washukiwa.
Waziri
Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV,
alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu
kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au
kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya.
“Niseme
kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo
ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama
nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje?
'Kwasababu
kwa vyovyote vile nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti
utanibana ntakwambia twende nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua
mnakuta hamna, si basi!
"Kwahiyo
nikawa na wasiwasi kwamba inawezekana kabisa nia ilikuwa njema lakini
nilidhani pangeweza kutengenezwa utaratibu bora zaidi ya namna ya
kuwapata, kwasababu hapa kuna watumiaji, kuna wauzaji na wale ambao
wanaleta sasa madawa ya kulevya,” alisema Nape.
Aliendelea, “Ukishughulika
na mtumiaji huyu ukadhani ndiye mhalifu wako unakosea, kwasababu huyu
ni muathirika na muathirika anahitaji dawa anahitaji huduma
ameshaathirika, hapa wahalifu wetu nikuanzia huyu anayemletea halafu
kuna huyu anayempa yule aliyemletea, sasa ili uwapate hawa wawili lazima
umtumie huyu vizuri ili akupeleke kwa hawa wawili. Lakini ukimkamata
huyu ukamtia ndani sasa hawa wawili watakimbia.”
“Kwahiyo
mimi nikaona kwamba tunaivuruga vita yenyewe, anayeingiza madawa ya
kulevya na anayesambaza kwa maana ya kuyauza, hawa ndiyo tatizo letu. Na
ndio maana nikasema hebu tutumieni busara, watu wakadhani nimepinga.
"Tena
mimi nilisema mara nyingi sana tumieni busara namna ya kuiendesha vita
hii. Madhara ya kutotumia busara katika vita hii ni makubwa sana,
kwasababu ukimweka huyu mtu mmoja ndani hawa wengine wataendelea
kuwaathiri wengine na ndiyo maana nasema hii vita tutumieni busara.
"Hii
vita ni ya kupigana kimya kimya kwasababu wanaofanya biashara hii
hawaifanyi hadharani wanafanya kwa kificho. Shughulika nao kwa kificho,
hii vita hakuna mahali ambapo wameshawahi pigana hadharani, tukitajana
hadharani hata wenye chuki watatajana humo humo,” alisisitiza.
0 Maoni:
Post a Comment