MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA TAIFA STARS AMEFARIKI DUNIA


Godfrey Bonny kiungo wa zamai wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefariki dunia alfajiri ya leo huko nyumbani kwao Mbeya.

February 2, 2017 mtandao huu uliandika habari ya kuumwa kwa Godfrey Bonny ambaye alikuwa amelazwa hospitali ya Rungwe-Tukuyu Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati akicheza soka, Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Mtandao huu unaungana na wadau wengine wa soka na michezo kwa ujumla, kutoa pole kwa familia ya Godfrey Bonny kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wetu.

R.I.P Godfrey Bonny, hakika tutaendelea kukumbuka kile ulichokifanya katika soka la Tanzania.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment