Picha kutoka library yetu
Katika hali isio kuwa ya kawaida ni baada ya wimbi la watu wanaojihusisha na vitendo vya kitapeli limeendelea kushika kasi katika wilaya ya kyela mkoani mbeya ,ambapo katika kata ya Ipinda wilayani humo kuna watu wanajifanya waganga wa kienyeji wanaodanganya watu kuwa wanatoa pesa za utajiri baada kujimba shimo maeneo ya makaburi na kisha kutegesha watu chini ya kaburi kwa madai kuwa ni mizimu.
Taarifa kutoka kwa wakazi maeneo hayo zimeeleza kuwa kuna kikundi cha utapeli kimeanzishwa , ambapo kimechimba shimo maeneo ya makaburini na kuweka mafuvu ya wanyama waliokufa kisha kukata chumba kwa pazia juu yake wanaziba huku ndani ya chumba katika shimo hilo anakaa mtu.
Wanapo kuwa na mteja anayerubunika kutaka utajiri anapelekwa makaburini wakidai wanaongea na mizimu ambapo wanakaa pembeni ya shimo hilo,kisha watu hao wanaomba mizimu na mtu aliye katika shimo anajibu na kutamka atoe mamilioni ya fedha kisha apewe utajiri ndani ya siku saba.
Siku chache zilizopita kuna mtu alipelekwa kwa mtindo huo makaburini na akatapeliwa zaidi ya milioni kumi na walipoendelea na kasi hiyo ya utapeli baadhi yao waliuawa,ambapo serikali wilayani humo imetangaza kiama kwa watu wanaoendesha vitendo hivyo.
0 Maoni:
Post a Comment