Dc Kasesela Akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji
Akizungumza katika kikao kilichowahusisha Watendaji wa Vijiji
pamoja na Wenyeviti wa Mitaa ambacho kilihudhuriwa naa Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa bwana Williamu Mafwele ambaye mwenyekiti wa kikao hicho alikua Mh Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambao walikutana kujadili maendeleo pamoja
na ufafanuzi wa kodi wa nyumba ambao utahusisha ubora wa nyumba.
Katika kikao hicho DC KASESELA amewataka Watendaji wa vijiji
kuto toa taarifa zozote zinazohusiana na hali ya Chakula katika Maeneo yao
kwani kumekua na taarifa ambazo sio rasmi zinahusisha mtu mmoja kua na njaa na
kujumuisha watu wote kua kuna njaa huku wengine wakitoa taarifa katika vyombo
vya habari kua kuna njaa.
“Kuanzia sasa, wiki iliyopita hata mwezi uliopita na
kuendelea Ni marufuku kutoa taarifa zozote zinazohusiana na Chakula kama
hujaambiwa na mkubwa wako, lete taarifa kwangu mimi, leta taarifa kwa Afisa
tarafa na leta taarifa kwa mtendaji kata halafu tutakaa kikao kujadili na
kuangalia kwa pamoja na kubaini kua kuna tatizo”. Alisema Kasesela
Aidha Kasesela akasema kua kweli kuna maeneo hayajapata mvua
na amepata taarifa kua kuna baadhi ya
maeneo Tembo amekula mazao na amepokea taarifa hizo kutoka kijiji cha Kiwele
kua Tembo amekula Mazao hivyo kwa vyovyote vile watu hao watahitaji msaada wa
chakula.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Wilaya YA Iringa akawataka
watendaji hao kuhakikisha wanawaelimisha wananchi wao kuhusu Utapia mlo na
haswa kulivalia njuga swala hilo ili kuweza kutokomeza kabisa utapiamlo na
watoto wanapata chakula bora.
“Mwaka jana sikutaka kuwasumbua lakini mwaka huu lazima
tuhakikishe watoto wote wanaoisha katika nyumba zote wanapata lishe iliyo bora,
Na niseme tu kua wengi wenu mnadharau kula Dona mimi jana nimepiga dona na ndio
maana mnaniona nina Afya njema kama hivi”. Alisema Kasesela.
Kasesela akawaambia wenyeviti wa Mitaa kua anatambua hali za
mazingira magumu wanayofanyia kazi nab ado wanayashughulikia ili wawe katika
hali nzuri huku akisema kua anachukia hali hiyo na akawaahidi kua analifanyia
kazi pamoja na Mkurugenzi.
0 Maoni:
Post a Comment