Star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya heshima ya Ballon d’Or kwa mara ya nne.
Ronaldo,31, aliisaidia Madrid kushinda Champions League msimu uliopita na alifunga magoli matatu kwenye michuano ya Euro yaliyoisaidia Ureno kutwaa taji la Euro 2016.
Tuzo hiyo imekuja baada ya kutwaa zingine tatu katika miaka ya 2008, 2013 na 2014.
“Sikuwahi kufikiria kwenye maisha yangu kama ningeshinda tuzo hii mara nne. Nashukuru, najivunia na nimefurahi,” amesema Ronaldo.
“Ninawashukuru wachezaji wenzangu wote, timu ya taifa, Ral Madrid, watu wote na wachezaji nilioshirikiana nao kushinda tuzo hii binafsi.”
Ronaldo sasa yupo nyuma ya mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ambaye ametwaa tuzo hiyo mara tano (2009, 2010, 2011, 2012 na 2015).
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga magoli 19 katika mechi 20 za Real Madrid na timu yake ya taifa akiongezea kwenye magoli yake 54 ya msimu uliopita.
Washindi wa Ballon d’Or tangu mwaka 2003.
2016: Cristiano Ronaldo | 2009: Lionel Messi |
2015: Lionel Messi | 2008: Cristiano Ronaldo |
2014: Cristiano Ronaldo | 2007: Kaka |
2013: Cristiano Ronaldo | 2006: Fabio Cannavaro |
2012: Lionel Messi | 2005: Ronaldinho |
2011: Lionel Messi | 2004: Andriy Shevchenko |
2010: Lionel Messi | 2003: Pavel Nedved |
0 Maoni:
Post a Comment