Kutoka na kilichotokea mwaka 2006 kwenye fainali za kombe la dunia kati ya Zidane na Marco Materrazi kimebaki kwenye historia ya kombe la dunia hadi leo.
Kwenye mazungumzo mbali mbali kuhusu kilichotokea pale uwanjani hadi Zidane akampiga kichwa cha kifua Marco Materrazi ilikua ni kutupiana matusi. Zidane alismea Marco alimtukana mama yake, Marco akasema alimtukana dada yake na sio mama yake.
Sasa hadi leo Marco Materazzi bado anandelea mambo ya hayo kwa mwenzako ambaye sasa hivi ana changamoto ya kuendelea kukiongoza kikosi cha Real Madrid.
Marco Materrazi ame post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha picha ambayo katuni kama Zidane ikipiga kichwa na yeye akiwa ameshika kombe la dunia juu.
Kuthibitisha zaidi kama ile picha ni Zidane, kuna picha ya Jogoo ambayo ndio nembo ya timu ya taifa ya Ufaransa.
Kwa hiyo maana yake ni kwamba Materrazi ameweka hiyo picha nyumbani kwake ikiwa ni kama ukumbusho wa tukio hilo ambalo halitakiwi kukumbukwa.
0 Maoni:
Post a Comment