July
14, 2016 Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe aliuacha rasmi ukapera
baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake. Leo December 27 2016 Zitto Kabwe
na mkewe wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm
Kulthum.
Zitto Kabwe amezitoa taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Ameandika:
''Mimi na Mke wangu mpendwa tumebarikiwa na Allah kupata mtoto wa kike.
Mtoto na mama yake wana afya njema kabisa, Mashaallah. Mtoto amezaliwa
saa moja na dakika 45 asubuhi leo Disemba 27, 2016''''.
''Binti
yetu ataitwa Josina - Umm Kulthum. Josina kwa heshima ya mwanamama
mpigania Uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO.
Umm Kulthum kwa heshima ya mama yangu mdogo na pia jina la binti wa
Mtume Muhammad (SAW)''
''Tunamshukuru mungu kwa Baraka hizi za mtoto Josina - Umm Kulthum Zitto''
0 Maoni:
Post a Comment