Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gaddafi’, alitoa pongezi hizo za mkoa wake jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema kuhusu uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mtoni Kijichi, Temeke, jijini Dar es Salaam, katika kinyang'anyiro hicho, CCM mkoa ilimteua Tausi Milanzi kupeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi huo utakaofanyika Januri 22, mwakani.
Akimsifu Rais, Simba alisema, “Rais Magufuli ameendesha vikao kwa muda mfupi, lakini kwa mafanikio makubwa na sisi kama CCM mkoa tutahakikisha tunashirikiana kwa karibu zaidi na vuiongozi wa Taifa walioteuliwa hivi karibuni,” alisema.
Alisema pamoja na Rais Magufuli kuendesha vikao hivyo kwa muda mfupi, lakini ameweza kutoa maamuzi mazito yenye lengo la kukijenga chama hicho kwa siku moja.
Simba alisema katika kipindi cha mwaka mmoja chini ya uongozi wake amefanya mengi mazuri ambayo kila mwanaCCM anapaswa kujivunia kwa kuwa ni utekelezaji wa chama hicho.
Aliongeza kuwa, pamoja na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho, kuonesha juhudi za kuijenga nchi kiuchumi, bado wapo watu wachache wanaomkwamisha kwa mambo mbalimbali ikiwemo kulipa kodi, hivyo kuwataka wanaokwepa kodi kulipa ili maendeleo ya Tanzania yapatikane kama yalivyo malengo ya Rais Magufuli.
0 Maoni:
Post a Comment